Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanzisha rasmi huduma ya upandikizaji mimba, utakaowawezesha wanawake na wanaume wenye matatizo ya kupata mtoto kwa njia ya kawaida. Njia hiyo ya kisayansi ni hatua ambayo inayokusudiwa kuleta mapinduzi katika tiba na kwa gharama nafuu katika taifa hilo la Afrika Mashariki.