Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameitaka Serikali kurudisha huduma za kijamii kwa wananchi wa Ngorongoro ambao wanaishi hifadhini kwa maisha yao yote.
Mbowe amesema kunyimwa huduma za kijamii kama afya, maji na elimu ni kinyume na haki za binadamu na Serikali inapaswa kutumia njia nyingine kuwaondoa kihiari na siyo kwa lazima.