Akiongea hivi karibuni na Shannon Sharpe kwenye ‘podcast’ ya Club Shay Shay, muigizaji Tyrese Gibson aliibua mjadala ambao ulitaka kujua ni nani kati ya marapa Snoop Dogg au Jay-Z ni maarufu zaidi duniani.
Mjadala huo wawili hao wakauhitimisha kuwa Snoop Dog ndiye Rapa mkubwa zaidi ya Jay Z.
TYRESE: Snoop ni gwiji… rapper mkubwa zaidi duniani… na huenda akatangaza yeye ni bilionea hivi karibuni.
SHANNON SHARPE: Sitashangaa.
TYRESE: Haupaswi kushangaa. Anamiliki biashara 732.