Majaliwa: Uvuvi waingiza mapato trilioni 2.9
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema sekta ya uvuvi inaingiza mapato ya Sh. trilioni 2.94 kwa mwaka na imekuwa ikikua kwa wastani wa asilimia 1.9. “Wastani wa uzalishaji wa samaki kwa mwaka hapa nchini unafikia tani 472,579, huku 429,168 sawa na asilimia 91 zikitokana na uvuvi wa kawaida wa kutumia vyanzo vya asili ndani ya bahari,…