Rapa wa Marekani Wiz Khalifa ambaye jina lake halisi ni (Cameron Thomaz), alikamatwa jana Julai 14 nchini Romania baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Bangi.
Rapa huyo, alikuwa Romania kwa ajili ya kushiriki kwenye tamasha la “Beach, Please!” lililofanyika kwenye pwani ya Costinesti na inaelezwa kuwa alionekana akivuta bangi wakati akiwa jukwaani.
Baada ya kukamatwa Khalifa alikutwa na zaidi ya gramu 18 za bangi, alihojiwa pamoja na watu wengine kadhaa na baadae kuachiliwa.