Marioo ajitoa kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume Tanzania.

marioo

Ikiwa ni siku moja imepita tangu waandaji wa Tuzo za muziki Tanzania (TMA) kutangaza majina ya wasanii watakaoshindania tuzo hizo kwa kipengele cha msanii bora wa kiume miongoni mwao akiwemo Marioo kupitia wimbo wake wa ‘Shisha’ msanii huyo ametangaza rasmi kujitoa kwenye tuzo hizo.

Marioo amefunguka hayo kupitia ujumbe aliounandika kwenye mtandao wa instagram baada ya kutoa taarifa za kuwania tuzo hizo huku akisema pamoja na kwamba anathamini na kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza na kuinua sanaa lakini hakubaliani na fitna za watu wachache.

Ikumbukwe,wasanii waliotangazwa kuwania kipengele cha msanii bora wa kiume ni Marioo kupitia ngoma ya ‘Shisha’, Diamond ‘Shu’, Harmonize ‘Single Again’, AliKiba ‘Sumu’ na mwisho ni Jay Melody na wimbo wa ‘Nitasema’.

Vigezo vya kushinda tuzo hizo kwa wasanii washindani waliotangazwa ni kupigiwa kura na mashabiki na tayari waandaji wa tuzo hizo wametangaza kufungua dirisha la kupiga kura kuanzia siku ya jumannne ya wiki ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *