HAWA HAPA WACHEZAJI WOTE WALIOBEBA TUZO ZA TFF 2023/24

Usiku wa tarehe 1 August 2024, katika jiji la Dar Es Salaam limefanyika moja kati ya tukio kubwa la kimichezo katika nchi ya Tanzania, nalo ni ugawaji wa tuzo kwa wachezaji waliofanya vyema katika msimu wa 2023/2024, Tuzo zinazofahamika kama TFF Awards ambapo zimefanyika katika ukumbi wa Super Dome.

Katika Usiku Huo wa ugawaji wa tuzo wachezaji mbalimbali walifanikiwa kuondoka na tuzo zao katika kutambua juhudi zao walizozifanya katika msimu, na hapa sokaleo.co.tz tumekuwekea wachezaji wote na tuzo walizoshinda, endelea kutembelea website yetu kwa kupata habari mbali mbali za kimichezo, au download app yetu hapo chini.

Mfungaji Bora wa Ligi

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ametangazwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Golikipa Bora, Kombe la Shirikisho (CRDB)

Mlinda mlango wa klabu ya Yanga Sc, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Michuano ya FA (CRDB FEDERATION CUP).

Diarra amewashinda Khomein Abubakar kutoka Ihefu (Singida Black Stars) na Mohamed Mustafa kutoka Azam Fc.

Golikipa Bora, Ligi Kuu Bara

Mlinda mlango wa Coastal Union, Ley Matampi ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara Msimu wa 2023/2024 akiwashinda Djigui Diarra wa Yanga na Ayoub Lakred wa Simba SC.

Beki Bora Ligi Kuu Bara

Beki wa Yanga Sc na Timu ya taifa ya Tanzania, Ibrahim Bacca ameshinda tuzo ya beki Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Kiungo Bora

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki raia wa Burkina Faso ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu bara msimu wa 2023-24 akiwashinda Kipre Junior wa Azam Fc na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam Fc.

Mchezaji Bora wa Tanzania, Anayecheza Nje

Nahodha wa mshambuliaji wa klabu ya Paok ya Ugiriki, Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa kiume wa Tanzania anayecheza nje ya Tanzania.

Mfungaji Bora (MVP) kombe la Shirikisho

Kiungo wa Azam Fc, Faisal Salum ‘Feitoto’ ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup 2023/24) kwa msimu wa 2023/24.

  • Mchezaji Bora Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) – Aisha Mnunka
  • Mfungaji Bora Ligi ya Wanawake – Aisha Mnunka
  • Kipa Bora Ligi ya Wanawake – Caroline Rufo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *