Jeshi la Israel limethibitisha lilimuua mkuu wa kijeshi wa kundi la wapiganaji wa Hamas, Mohammed Deif, katika shambulio lililotumia ndege za kivita katika eneo la Khan Yunis tarehe 13 ya mwezi Julai.
Madai ya Israeli kumuua Deif yamekuja ikiwa imepita siku moja baada ya kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran.
Israeli imesema Deif alipanga na kutekeleza shambulio la tarehe 7, Oktoba, 2023 na kuua watu 1,197.