Maelfu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa Hamas aliyeuawa

Maelfu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, nchini Iran ambaye aliuawa katika shambulizi mjini Tehran siku ya Jumatano.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, anaongoza sala hiyo kabla ya kiongozi huyo kuzikwa nchini Qatar.

Vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maafisa wa Iran wakisema kiongozi huyo mkuu ameamuru shambulio la moja kwa moja dhidi ya Israel, na ndio chanzo cha shambulio lililotokea nchini Iran.

Israel haijatoa maoni yoyote kuhusu mauaji hayo moja kwa moja.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake imetekeleza “pigo kali” kwa maadui zake katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa kamanda mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon saa chache kabla ya shambulio la Tehran.

Alionya Waisrael kwamba “bado kuna changamoto siku za usoni”, huku hofu ya mzozo mkubwa katika Mashariki ya Kati ikiongezeka

“Tangu kutokea kwa shambulizi Beirut, tumesikia vitisho kutoka pande zote,” alisema kwenye ujumbe uliopeperushwa kwenye Televisheni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya dhidi ya “kuongezeka kwa hatari” kwa uhasama katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *