Katibu wa Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Dar es salam (Kichama) Ndugu CPA Amos Makalla Leo tarehe 14 Julai 2024 ameanza Ziara Wilaya ya Ubungo yenye Majimbo Miwili ya Kibamba na Ubungo na kuanzia Kibamba.
Mwenezi Makalla ameanza ziara hiyo kwa kukagua miradi mbalimbali akianzia katika Shule ya Kisasa ya Mchepuo wa Sayansi ya Wasichana kuanzia kidato cha Kwanza mpaka cha Sita DAR ES SALAAM GIRL HIGH SCHOOL,Mradi unaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4.
Pia alikagua wa Mradi wa Tenki la Maji la Ujazo wa Lita 6000 lilipo Mshikamano Jimbo la Kibamba Wilaya ya Ubungo.
Makalla aliwaambia wanafunzi wa shule hiyo ” pongezi zote zimuendee Dkt Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kuwekeza Kwa Wananchi tukianzia na Shule hii ni ya Mfano Kwa Mkoa wa Dar es salam na Tanzania nzima kwa Ujumla kazi iliyobaki ni kwenu Wanafunzi na Walimu kuhakikisha tunapata Matokeo Mazuri”
Aidha katika Mradi wa Maji alitoa rai kwa Mamlaka ya Maji Dar es Salaam DAWASA “hakikisheni mnafikisha Maji pembezoni mwa Jiji la Dar es salam iwe Sawa na Mijini kwani Wananchi wanaimani kubwa na CCM mnapofanya Vibaya mnawagombanisha na Chama chao Wakati Mhe Rais Dkt Samia ameshafanya utekelezaji, kazi imebaki kwenu kufikisha Maji Kwa Wananchi wa Jimbo la Kibamba na Wilaya ya Ubungo Kwa Ujumla”