Habari Kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 21, 2024
Pitia kurasa za mbele za magazeti ya Tanzania kitaifa na kurasa za kimichezo pamoja na gazeti la Michezo ya leo July 21, 2024 na ujipatie nakala yako kwa undani wa habari.
Pitia kurasa za mbele za magazeti ya Tanzania kitaifa na kurasa za kimichezo pamoja na gazeti la Michezo ya leo July 21, 2024 na ujipatie nakala yako kwa undani wa habari.
Katika hali ya kushangaza wafuasi wa Chama cha Republican wameonekana wakiwa wamevaa bendeji feki masikioni kama aliyokuwa amevalishwa Trump baada ya kujeruhiwa na risasi kwenye sikio lake. Wanachama hao wanasema wameamua kuvaa hivyo kama njia ya kumuunga mkono Trump kwenye mbio zake za kugombea Urais wa Marekani ikiwa ni siku chache baada ya kunusurika kuuawa.
Klabu ya Azam imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji Mamadou Samake kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwa miamba ya Algeria, CR Belouizdad. Samake (24) raia wa Mali anafunga rasmi usajili wa Wanalambalamba hao kwenye dirisha hili kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 na anatarajia kujiunga na kambi ya timu hiyo nchini Morocco muda…
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imekubali ombi la klabu ya Yanga ya kusogezwa mbele kwa muda wa kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanachama wa klabu hiyo kuhusu uhalali wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo Awali Mahakama hiyo iliamuru Uongozi wa klabu ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi…
Klabu ya APR Fc ya Rwanda imetinga fainali ya CECAFA Kagame Cup kufuatia ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Al Hilal ya Sudan baada ya dakika 90 za mchezo na zile 30 muda wa ziada kumalizika bila bao kabla ya Mabingwa hao mara tatu wa kombe hilo kufunga penalti zote huku Al Hilal ikikosa penalti…
UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa wachezaji wapya ambao wametambulishwa watafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wengine katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa. Simba imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kujipanga kufanya vizuri. Ipo wazi kwamba katika anga la kimataifa Simba itashiriki Kombe la Shirikisho…
NAHODHA msaidizi wa Yanga Dickson Job ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mechi zote za kirafiki kimataifa ambazo watacheza nchini Afrika Kusini ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya msimu wa 2024/25. Ipo wazi kwamba Job ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi anaingia kwenye orodha ya mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya Yanga msimu uliopita alifanya hivyo mbele ya KMC mchezo…
Waandamanaji nchini Bangladesh wamevamia gereza siku ya Ijumaa na kuwaachilia “mamia” ya wafungwa kabla ya kulichoma moto gereza hilo, afisa wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP. “Wafungwa wametoroka gereza na waandamanaji wamechoma moto gereza”, afisa wa polisi amesema, akizungumza kwa sharti la kutotajwa. “Sijui idadi ya wafungwa waliotoroka lakini itakuwa mamia,” ameongeza….