Rais Samia awateua Prof. Assad na Balozi Ombeni Sefue

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi (Presidential Commission on Tax Reforms) na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Aidha, wajumbe wa Tume walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Prof. Florens Luoga Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

Prof. Mussa Juma Assad Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

Bw. Leonard Mususa Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania;

CPA. Aboubakar Mohamed Aboubakar Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU);

Balozi Mwanaidi Sinare Maajar Mshauri wa Masuala ya Sheria;

Bw. David Tarimo – Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa ldara ya Ushauri wa Kodi, PwC;

Balozi Maimuna Kibenga Tarishi Katibu Mkuu Mstaafu;

Bw. Rished Bade Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Tarehe 29 Julai, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *