Tuzo hazina “link” msipotoshwe ; TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ‘TFF Awards 2024’ limethibitisha kuwa halfa za kukabidhi tuzo hizo zitafanyika Agosti Mosi, 2024 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki, Dar es Salaam huku ikionya kuwa tuzo hizo hazina vigezo vya mashabiki kupiga kura kama ambavyo imekuwa ikipotoshwa mitandaoni.

“Tunapenda kusisitiza kuwa katika vigezo hivyo, hakuna cha washabiki kupigia kura walioteuliwa kuwania tuzo hizo (nominees).

“Hivyo, tunawaomba washabiki na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla kupuuza kiunganishi (Link) kinachosambazwa mitandaoni kuwataka wapige kura kuchagua washindi”.

“Pia tunawataka wale wote wanaosambaza kiunganishi hicho kinachopotosha kuacha kufanya hivyo mara moja, kuendelea kusambaza ni kutenda kosa.” ilieleza taarifa ya TFF kwa umma.

Washindi katika vipengele mbalimbali watatunukiwa tuzo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na TFF chini ya Kamati yake ye tuzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *