Polisi kuwakamata Chadema wanaoenda Mbeya kwenye Kongomano

polisi

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Awadhi Juma Haji amewaagiza makamanda wa Polisi wa Mikoa (RPC) kufanya ukaguzi kwenye mabasi yanayoelekea jijini Mbeya kwenye kongamano la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuwachukua hatua wahusika.

Haji ametoa maagizo hayo leo Jumapili, Agosti 11, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya. Ni baada ya kongamano hilo lililopangwa kufanyika kesho Jumatatu, Agosti 12, 2024, Viwanja vya Ruanda Nzomve kupigwa marufuku na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limepanga kufanya kongamano hilo katika kilele cha siku ya vijana duniani ambapo wageni mbalimbali wamealikwa akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe Makamu wake Tundu Lissu na Rais wa Chama cha Mawikili Boniphace Mwabukusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *