Mourinho aanza na kadi Uturuki klabu yake ikishinda

Licha ya klabu yake mpya ya Fenerbahce kuanza na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uturuki (Turkish Super Lig) dhidi ya Adana Demirspor, ilimchukua dakika 19 tu Jose Mourinho kuanza ligi hiyo na kadi baada ya kuadhibiwa kwa kadi ya njano alipozozana na mwamuzi wa akiba.

Kocha huyo aliyejipachika jina la The Special One ambaye kwa sasa ni bosi wa Fenerbahce alikasirishwa baada ya uamuzi kwenda kinyume na timu yake, ambapo alianza kupiga kelele na kumfokea mwamuzi wa akiba.

Jambo hilo lilimfanya Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United, Real Madrid, Inter Milan, FC Porto na Tottenham aonyeshwe kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo Atilla Karaoglan.

Goli la pekee la Fenerbahce lilifungwa na aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City na AS Roma Edin Dzeko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *