Beyonce kumburuza Trump mahakamani.

Mwanamuziki wa Marekani Beyonce ameripotiwa kumfungulia mashtaka Rais wa zamani wa Marekani ambaye kwa sasa yupo kwenye kampeni za kurejea kwenye kiti hicho Dolald Trump kufuatia kutumia wimbo wake wa ‘Freedom’ bila ridhaa yake.

Siku ya Jana Trump mtu mmoja aliyepo kwenye timu ya kampeni ya Trump Steve Cheung alichapisha kipande cha video kwenye mtandao wa X chenye sekunde 13 kilichomuonesha Trump akishuka kwenye ndege huko Michigan huku akitumia wimbo wa Beyonce aa 2016 ‘Freedom’ kwenye video hiyo.

Hata hivyo, muda mchache baadae video hiyo ilifutwa kwenye ukurasa huo wa mtandao wa X ikiwa ni muda mchache baada ya kuzuka taarifa za mmiliki wa wimbo huo Beyonce kutaka kumfungulia mashtaka mwanasiasa huyo.

Beyonce tayari alitoa kibali kwa mpinzani mkubwa wa Trump ambaye ni Kamala Harris kuutumia wimbo huo kwenye kampeni zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *