Israel yamuua kiongozi wa kijeshi wa fatah nchini Lebanon

Khalil Al-Maqdah, kiongozi wa kijeshi wa Fatah kutoka Palestina, aliuawa Jumatano ya jana Agosti 21 katika shambulio la Israeli lililofanyika nchini Lebanon.

Khalil aliuawa akiwa ndani ya gari yake karibu na kambi za Wapalestina zinazopakana na mji wa Saida, kusini mwa Lebanon.

Jeshi la Israel, kwa upande wake lilitangaza kwamba lilimuua ‘gaidi’ ambaye alikuwa anafanya kazi na Iran.

“Alihusika katika shughuli za kigaidi na biashara ya silaha katika Ukingo wa Magharibi” lilisema jeshi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *