Kupoteza kazi kwa Waziri kwaibua shangwe, vijana wakata keki kusherehekea

Kupoteza kazi kwa aliyekuwa Waziri wa Barabara wa nchini Kenya, Kipchumba Murkomen, kumekuwa sherehe kwa baadhi ya vijana almaarufu kwa jina la Gen Z wa huko North Rift nchini Kenya (iliko ngome ya waziri huyo).

Ilikuwa furaha kwa baadhi ya vijana hao walioamua kufanya sherehe ya kukata keki kumshukuru Rais William Ruto kwa kumwachisha kazi Waziri Murkomen pamoja na mawaziri wengine 22 baada kuvunja baraza la mawaziri wiki iliyopita kutokana na shinikizo za vijana wa Gen Z.

Gazeti la #TaifaLeo limeripoti kuwa sherehe hiyo ya kukata keti ilifanyika mjini Eldoret karibu na jengo ambalo linadaiwa kumilikiwa na Waziri huyo, huku vijana hao wakitamka maneno kwa lugha ya Kikalenjin ambayo yalionekana kama tambiko la kulaani hatua yeyote ya kumrudisha Murkomen kazini hasa katika baraza la mawaziri.

Akiongea kwa niaba ya vijana wenzake, Rais wa vuguvugu la vijana wa North Rift, Kelvin Kipleting alisema;

“Murkomen amekuwa na tabia ya kutudharau na kutukejeli sisi kama vijana, leo hii tunakata keki ya kusherehekea uamuzi wa busara wa rais huku tukimkaribisha kujiunga na kundi la vijana wasiokuwa na kazi ili hata yeye ahisi vile tumemkuwa tukisikia wakati alikuwa akituonyesha madharau na kutojali,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *