Mume achoma vyeti vya mkewe baada ya kugundua anamcheat

Mwanamume mwenye hasira amefichua kwamba alimuadhibu mkewe kisiri baada ya kugundua anachepuka na wanaume wengine.

Mume huyo alisimulia kwamba aligundua mkewe alichepuka na wanaume wawili kwa kufanya nao mapenzi kwa pamoja siku iliyopita na akaamua kumfanyia kitendo ambacho hatosahau.

Ili kujiridhisha zaidi na adhabu yake, aliidukua simu yake na kuiba kila senti iliyokuwa kwenye akaunti zake za pesa bila mke kujua nini kinaendelea.

Hakuishia hapo, kisha alichukua vyeti vya mkewe vyote na kuviteketeza moto na baadae kujifanya hajui vilipotelea wapi.

Hadithi yake ilitumwa kwa X zamani twitterna influencer @Wizarab10 kama ujumbe usiojulikana na iliwakasirisha watu.

Mume huyo alitetea hatua hiyo akisema kwamba yeye ni mmoja wa watu wanaoamini katika falsafa ya kwamba hakuna kosa linalostahili kupita tu bila kuadhibiwa.

“Nimegundua kwamba mke wangu alifanya threesome jana, hivi sasa hajui kama niligundua. Mimi pia kwa upande wangu naamini kwamba katika kila tukio, lazima kuna madhara. Simu yake imedukuliwa na salio lote bila yeye kujua. Vyeti vyake pia vimetoweka, vimechomwa,” alisema mume huyo.

Hili lilivutia maoni kinzani baadhi wakimtuhumu kwa kufanya hivyo kama njia ya kulipa kisasi huku wengine wakimpongeza kwa kumpa funzo ambalo hatokuja kulisahau.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *