APR ya rwanda yatinga fainali CECAFA

apr

Klabu ya APR Fc ya Rwanda imetinga fainali ya CECAFA Kagame Cup kufuatia ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Al Hilal ya Sudan baada ya dakika 90 za mchezo na zile 30 muda wa ziada kumalizika bila bao kabla ya Mabingwa hao mara tatu wa kombe hilo kufunga penalti zote huku Al Hilal ikikosa penalti ya mwisho.

FT: APR Fc 🇷🇼 0-0 🇸🇩 Al Hilal (P 5-4)

APR Fc imetangulia fainali kumsubiri mmoja kati ya Al Wadi ya Sudan dhidi ya Red Arrows Fc ya Zambia huku Al Hilal ikisubiri timu itakayofungwa kwenye nusu fainali ya pili kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.

Mshindi wa Michuano hiyo ya kikanda inayodhaminiwa na Chama cha Soka cha Sudan (SFA), Bandari ya Dar kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania, Azam TV na Rais wa Rwanda, Paul Kagame atajinyakulia dola za Marekani 30,000, mshindi wa pili dola 20,000 na wa tatu atashika nafasi ya 10,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *