Marekani inaamini Iran itaanza kuitwanga Israel muda wowote kuanzia leo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewaambia viongozi wenzake wa G7 kwamba Washington inaamini kwamba mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yanaweza kuanza ndani ya saa 24 hadi 48 zijazo, huku Marekani ikiendelea na juhudi za kutuliza hali ya wasiwasi katika eneo na kujaribu kuzuia vita.

Marekani inaamini kuwa shambulio la Iran la kulipa kisasi haliwezi kuepukika baada ya kuuawa kwa maafisa wakuu wa Hezbollah na Hamas wiki iliyopita.

Blinken amesema Marekani haijui muda sahihi wa shambulio lililopangwa la Iran, lakini inaamini kuwa linaweza kuanza mapema Jumatatu (Leo).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *