Baada ya miaka 6 ya ndoa hatimaye Justin Bieber na mkewe wajaliwa mtoto.

Ikiwa ni miaka sita imepita tangu walipofunga ndoa kwa siri huko New York mwaka 2018 Mwanamuziki Justin Bieber na mke wake Hailey hatimaye wamefakiwa kupata mtoto wao wa kwanza aitwaye Jack Blues Bieber.

Bieber amethibitisha kupata mtoto huyo siku ya jana Ijumaa Agosti 23 kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuchapisha picha ya mguu wa mtoto huku akimkaribisha nyumbani.
Baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Marekani akiwemo Kim Kardashian wamempongeza Bieber na mkewe kwa baraka hiyo ya kuongeza mwanafamilia mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *