BILIONI 10.7 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA ZA NDANI KWENYE JIJI LA DAR

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kutumia Sh bilioni 10.7 za mapato ya ndani kujenga zaidi ya kilomita 6 za barabara kwa kiwango cha lami na zege.

Zabuni za ujenzi wa barabara hizo zilitangazwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 na Julai 15,2024 jiji hilo limesaini mikataba na wakandarasi waliopewa kazi hizo.

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mrisho Satura, amesema wamekuwa wakitenga asilima 10 ya mapato ya ndani kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa mujibu wa Satura, katika mwaka wa fedha 2022/2023 walikusanya Sh bilioni 81 lakini mwaka 2023/2024 wamekusanya Sh bilioni 111.7 ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 30.

“Tutaweka nguvu kubwa katika usimamizi wa mapato ili kuongeza ukusanyaji na kujenga barabara nyingi zaidi, tunawaomba wakandarasi muwe waadilifu fedha hizi ni za wananchi na zimetafutwa kwa jasho kubwa, mjisimamie wenyewe kazi zifanyike kwa kasi,” amesema Satura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *