Daftari la kuandikia mistari ya wimbo la Rapa wa Marekani Lil Wayne ambalo alikuwa akilitumia mwaka 1999 wakati akiwa na umri wa miaka 17, sasa linauzwa kwa $5M (Sawa na shilingi Bilioni 13.5 za kitanzania)
Inaelezwa kuwa Daftari hilo lilipatikana kwenye gari la Cash Money Records, limeharibika kidogo kutokana na maji kutoka kwenye Kimbunga cha ‘Katrina’ lakini bado ni kipande cha historia ya muziki wa hip-hop.