Harusi ya mtoto wa bilionea wa bara la Asia Mukesh Ambani, Anant Ambani na binti wa mfanyabiashara wa maduka ya dawa wa India Radhika Merchant, iliyofungwa siku ya jana katika jiji la Mumbai Nchini humo inaendelea kuwaacha watu midomo wazi baada ya kubainika kuwa gharama zilizotumika kwenye harusi hiyo ni zaidi ya Trilioni 1.6 za kitanzania.
Sherehe za harusi hiyo zinaendelea huko Mumbai zikudhuriwa na matajiri mbalimbali wakiwemo wasanii wakubwa na wanasiasa kama Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, Tajiri Bill Gates,Mark Zuckeberg na wengine wengi.
Msanii kutoka Nigeria Rema ni miongoni mwa wasanii waliolikwa kwenye harusi hiyo na tayari ameshapanda jukwaani kutumbuiza huku ikidaiwa kuwa amelipwa Bilioni 7.9 kwa ajili ya kutumbuiza wimbo mmoja pekee.
Hafla za harusi zilianza na sherehe mnamo mwezi machi na huwenda zikaendelea kwa siku kadhaa huku sherehe kubwa ya mapokezi ikipangwa kufanyika siku ya Jumatatu.