Harusi ya mtoto wa Bilionea wa India yatikisa Duniani.

Baada ya harusi ya msanii Davido kutikisa Afrika hivi karibuni harusi nyingine inayoendelea kukamata vichwa vya habari duniani kwa sasa ni harusi ya mtoto wa bilionea wa India Mukesh Ambani anayeitwa Anant Ambani na mpenzi wake Radhika Merchant kutokana na ukubwa wa harusi hiyo.

Harusi hiyo ya kifahari inayohusisha watu maarufu duniani kama vile Shah Rukh Khan, Salman Khan, Deepika Padukone, na Amitabh Bachchan, Kim Kardashian, Mike Tyson, Adele, John Cena, Justin Bieber, Mark Zuckerberg, Khloe Kardashianna wengineo imefungwa hii leo huku Sherehe zikiendelea huko Mumbai nchini India.

Kabla ya harusi hiyo kulikuwa na matukio ya yaliyojumuisha sherehe kubwa mjini Jamnagar, ambapo Rihanna alifanya onesho la kusisimua. Pia, familia ilifanya sherehe nyingine ya kifahari nchini Italia iliyohudhuriwa Justin Bieber.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *