Jeshi La Polisi Mkoa Wa Simiyu Lakamata Watu Watano Kwa Tuhuma Za Kuwaua Watu Wawili

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limewakamata watu watano kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi kwa kuwakamata na kuwaua watu wawili kisha kuteketeza miili yao kwa moto.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Edith M. Swebe, mnamo tarehe 20 Septemba 2024, waliouawa ni Ntawa Limbu, Msukuma mwenye umri wa miaka 32, mkulima na mkazi wa Mtaa wa Buzunza, pamoja na mwenzake anayejulikana kwa jina moja la Suma.

“Chanzo cha kufanya uhalifu huo wa kujichukilia sheria mkononi ni kwamba inasemekana marehemu hao walikuwa wanamiliki mali zinazosadikika kuwa ni za wizi mara baada ya taarifa kumfikia mhanga aliyewahi kuibiwa aliweza kuhamasisha kundi la vijana waendesha pikipiki maarufu bodaboda na kuanza kuwatafuta watuhumiwa ambao kwa sasa ni marehemu”, imeeleza taarifa ya polisi.

Aidha Jeshi la Polisi limekemea vikali vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi, likieleza kuwa ni kosa la jinai. Upelelezi wa tukio hili unaendelea ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe na watuhumiwa wafikishwe mahakamani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *