Mama yangu alinipigia pande kwa mchumba wangu – Lady Gaga

Mwanamuziki nyota wa Marekani Lady Gaga, ameweka wazi kuwa mama yake mzazi ndiye aliyemtambulisha kwa mchumba wake wa sasa, Michael Polansky.

Gaga mwenye umri wa miaka 38 alifichua hayo katika mahojiano aliyoyafanya na Jarida la Vogue hivi karibuni.

Kwa mujibu wa msanii huyo, mama yake aliwahi kumtaarifu kipindi cha nyuma kuwa anamtafutia mume, lakini hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba angeweza kupata mwanaume sahihi kwa ajili yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *