Kutoka Nigeria mwanamuziki, Michael Adebayo Olayinka, almaarufu kwa jina la Ruger, amefunguka kuhusu undani wa maisha yake ya kimapenzi.
Msanii huyo kipenzi cha wadada, amewashtua wengi kwa kusema ‘hawezi kupenda tena’ kwasababu maisha yake ya mapenzi yameharibiwa na hivyo anashindwa kupata hisia.
“Maisha yangu ya mapenzi yameharibika … siwezi kupenda tena. Moyo wangu ni baridiiii. Sijisikii chochote tena,” Ruger alilalamika.
Itakumbukwa miezi michache iliyopita Ruger aliwahi kunukuliwa akisema anaweza kupenda wanawake watano kwa wakati mmoja.