MWANDISHI WA HABARI KENYA APIGWA RISASI AKIWA KWENYE MAJUKUMU YAKE

mwanahabari apigwa risasi

Mwandishi wa habari wa Catherine Wanjeri Kariuki anayefanya kazi katika kituo cha Kameme TV kilichopo chini ya Mediamax Limited, amepigwa risasi na polisi wakati akiwa kwenye majukumu yake katika mji wa Nakuru nchini Kenya, akiripoti maandamano yanayoongozwa na vijana wanaofahamika kama Gen Z yaliyodumu kwa wiki kadhaa yakimshinikiza Rais William Rutto kuachia madaraka.

Akiwa amevalia sare rasmi za wanahabari na alikuwa amesimama pembezoni mwa barabara alipigwa risasi tatu zilizolenga kwenye paja la mguu wake, wakati maafisa wa kiusalama wakikabiliana na waandamanaji na baada ya kupigwa risasi kundi la vijana wa Genz lilijitokeza kumsaidia na kumkimbiza katika Hospitali ya Valley.

Wakati huo Wanahabari mjini Nakuru waliandamana barabarani leo kukashifu kupigwa risasi kwa mwandishi mwenzao Catherine Kariuki. Walibeba mabango yenye ujumbe kama vile “polisi wauaji wa kukataa”, “haki kwa Cate”.

Baraza la Wanahabari Kenya MCK na Baraza la Mawakili Kenya LSK wamepinga vikali suala la maafisa wa usalama wa Nchi hiyo kutumia nguvu wakati wa kukabiliana na waandamanaji huku wakitumia silaha na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia.

MediaMax ni kampuni inayomiliki vyombo vya habari zaidi ya kimoja Nchini humo ikiwemo K24 TV ,Milele FM pamoja na kituo cha redio na Runinga cha lugha ya Kikuyu, Kameme FM na Kameme TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *