Nampenda sana Wizkid – Nicki Minaj

Kutoka nchini Marekani, Malkia wa Rap Nicki Minaj ameeleza jinsi anavyovutiwa na mwanamuziki wa Nigeria, Ayodeji Balogun, maarufu kwa jina la Wizkid.

Akiongea hivi majuzi kwenye kipindi cha #StationHead, Nicki alisema ana ‘upendo na heshima nyingi’ kwa Wizkid.

Minaj alimuelezea staa huyo wa ngoma maarufu ya ‘Ojuelegba’ kama mtu mtulivu na mwenye akili nyingi.

“Wizkid ni mtu poa na ana busara sana, ninampenda na kumheshimu sana.” alisema Minaj.

Minaj anasema alikutana na WizKid kwa mara ya kwanza alipokuwa akirekodi albam yake ya ‘Queen’ mwaka 2018 katika studio huko Queens, New York.

Licha ya tetesi za miaka mingi za kuwepo kwa ushirikiano wa kazi kati ya wawili hao lakini bado hawajatoa ngoma yoyote kuthibitisha hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *