Ole wenu Diamond akiwa tajiri namba 1Duniani mniite chawa.

Kauli ya mwanamuziki wa bongofleva Diamond Platnumz ya kuweka wazi ndoto yake ya kuwa tajiri namba moja Duniani imezua gumzo Nchini na kuibua mijadala mbalimbali huku wengi wakishangazwa na ndoto hiyo ya staa wa bongofleva.

Siku ya jana mtangazaji maarufu Mwijaku aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram akionekana kukosoa maneno hayo ya Diamond huku siku ya leo msanii Ommy Dimpoz ameibuka na jambo jingine jipya akiwataka mashabiki na wadau mbalimbali kutomuita chawa endapo Diamond atakuwa tajiri namba moja duniani.

Ommy Dimpoz amechapisha picha yake ya zamani akiwa na Diamond akiambatanisha na ujumbe ufuatao“Jamani Watanzania nadhani mmeona line nimetoka nayo mbali sana ole wenu akiwa tajiri namba moja tukiwa tunakula piza kwenye private jet mniite chawa, na tajiri kaniahidi atanikopesha niinunue Yanga” amendika Dimpoz

Ikumbukwe kuwa ndoto hiyo ya kuwa tajiri namba moja duniani Diamond aliisema wakati wa uzinduzi wa tamasha la Wasafi Festival.

“Ndoto yangu kubwa katika maisha ni kuwa tajiri namba moja duniani, ndio ndoto yangu na ninakuthibitishia kwamba nitakuwa tajiri namba moja duniani. Kwa sababu kwangu mimi naamini kila kitu kinawezekana, na ninawahakikishia kuwa mtanzania nitakayewakilisha taifa kwa kuwa tajiri namba moja duniani” alisema Diamond

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *