Penzi jipya la Jux lamtesa EX wake.

Aliyewahi kuwa mpenzi wa msanii wa muziki wa bongofleva Juma Jux mwanadada Karen Bujulu ameonekana kuumizwa na penzi jipya la msanii huyo kutokana na kile alichokichapisha kwenye ukurasa wake wa instagram muda mfupi baada ya Jux kuchapisha picha akiwa na mpenzi wake mpya raia wa Nigeria Pricila Star.

 

Jux ambaye hivi karibuni amekuwa akitajwa kuwa kwenye mahusiano na mrembo mwingine kutoka Nigeria aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo ambaye waliachana kimya kimya huku siku ya jana akichapisha picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mpenzi wake huyo mpya miongoni mwa hizo picha mojawapo mpenzi wake alikuwa ameshika glass yenye kinywaji.

 

Muda mfupi baada ya Jux kushare picha hizo mpenzi wake wa zamani alienda kwenye ukurasa wake wa instagram na kuchapisha picha ya glass yenye kinywaji iliyoambatana na ujumbe uliosomeka ‘Old fashioned’ ikiwa ina maana mtindo wa zamani au zilipendwa jambo ambalo baadhi ya watu wameihusianisha post hiyo na kile alichokuwa amekichapisha mwanamuziki Jux.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *