Rais Mstaafu CAF afariki siku kabla ya ‘Birthday’ yake

Aliyekuwa Rais wa CAF afariki dunia saa chache kabla ya kusheherekea ‘birthday’

Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Hayatou raia wa Cameroon amefariki dunia leo Agosti 8, 2024 akiwa jijini Paris, Ufaransa na ikiwa imesalia saa chache kabla ya kusheherekea kutimiza miaka 78 kesho Agosti 9.

Rais huyo ndiye aliyeongoza muda mrefu shirikisho la soka Afrika kuanzia 1988 hadi 2017.

Pia, amewahi kuliongoza shirikisho la soka Cameroon kuanzia 1986 – 1988 na 2015 – 2016 akawa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa muda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *