Sasa Itakuaje ?…!Mama Dangote amuambukiza Uncle Shamte Maradhi.

Sa Itakuaje…? Mume wa Mama Dangote mama mzazi wa Diamond Platnumz leo hii amefunguka  kuwa mwanamama huyo amempa maradhi  baada ya vipimo kutoka.

Uncle Shamte kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe huku akiambatanisha na picha ya Mama Dangote unaosemeka kama ifuatavyo…

Majibu ya vipimo vyote vinaonesha ya kwamba MARADHI yangu ni wewe tu.

1) Mganga kanishauri niwe nakunywa kikombe kimoja cha mate yako kila asubuhi…..

2) Kasema kila mtu ninayeongea naye LAZIMA nikutaje wewe mara 400 ata kama mada haihusiani…

3) Wadudu wa upendo wamezidi kwenye kichwa changu ndo maana nywele zimepotea….

4) Ili mapigo ya moyo wangu yaende sawa niwe nakupa 99 elfu kila kwenye laki 1 ninayoipata….

Uncle Shamte amemaliza kuandika kwa neno NAKUPENDA ❤️ aliloandika kwa herufi kubwa akithibitisha na kuweka wazi hisia zake juu ya Mama Dangote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *