TRUMP AONEKANA KWA MARA YA KWANZA HADHARANI HUKU AKIWA NA BANDEJI

trump

Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump amehudhuria mkutano wa chama chake cha Republican akiwa na bandeji sikioni na kukaribishwa kwa shangwe na wafuasi wa chama chake.
Hii ni mara ya kwanza kwa mgombea huyu wa Urais kuonekana kwenye hafla kubwa ya umma tangu kutokea kwa jaribio la mauaji dhidi yake siku ya Jumamosi.

Baada ya Trump kuingia kweye mkutano huo wafuasi wa chama chake cha Republican walikuwa na furaha iliyopitiliza huku wakiimba….

“U-S-A, U-S-A, U-S-A, U-S-A, U-S-A”
huku wakirusha ngumi hewani,
ikumbukwe kuwa Trump alionyesha ngumi hewani alipokuwa anashuka jukwaani baada ya kupigwa risasi huko Pennsylvania.
Wengine waliokuwepo ni pamoja na wanafamilia, kama vile wanawe Eric na Donald Jr.
Rais huyo wa zamani alionekana kutabasamu na kupiga makofi wakati wote wa hotuba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *