Hasbulla Magomedov ni staa mkubwa kwenye mitandao ya kijamii anayetokea Dagestan huko nchini Urusi.
Alipata umaarufu mwishoni mwa 2020 kwa vichekesho vyake kwenye Instagram kabla ya umaarufu wake kuongezeka alipoanza kutumia TikTok mwaka 2021 na amekuwa akialikwa sehemu mbalimbali duniani.
Ukimuangalia jinsi alivyo unaweza kudhani ni mtoto wa miaka 4, lakini Hasbulla aliyezaliwa mwaka 2002 ana miaka 22 kwa sasa.
Kingine cha kushangaza Hasbulla ana sauti kama ya mtoto wa miaka 4.
Hasbulla ana ugonjwa wa kimaumbile ambao umeathiri ukuaji wake