Maelfu ya wananchi Nchini Nigeria wamejitokeza katika maeneo mbalimbali kufanya maandamano ya amani waliyopanga kuyaanza leo Agosti 1 hadi 10 2024 wakipinga mfumuko wa bei kama chakula,maji, mavazi na utawala mbaya wa Rais wao Bola Ahmed Tinubu.
Katika maandamano hayo yanayoendelea hii leo baadhi ya waandamanaji wamechoma moto jengo la hifadhi ya viwanda vya kidigitali la Tume ya Mawasiliano ya Nigeria (NCC) lililopo katika Jimbo la Kano.
Waandamanaji hao walivamia jengo hilo na kuiba vifaa vingi vya ofisini kama vile viti, monitors, na vifaa vingine kabla ya kuliteketeza jengo hilo kwa moto.