Zelensky aomba ruhusa ya kuipiga urusi kwa makombora ya magharibi

Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky ametoa wito kwa washirika Katika mkutano na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na baraza lake la mawaziri, kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za Magharibi katika ardhi ya Urusi.

“Muhimu kwa hili ni silaha za masafa marefu. Tafadhali washawishi washirika wetu wengine kuondoa vizuizi, “Zelensky alimueleza Bw Starmer, akimaanisha kuruhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa silaha za Magharibi kwenye eneo linalotambuliwa la Urusi bila vizuizi.

Alipopokelewa na mwenyeji wake katika makazi ya Waziri mkuu wa Uingereza, Zelensky aliishukuru Uingereza kwa msaada na mshikamano wake na Ukraine.

“Asante kwa mwaliko na kunipa heshima ya kuwa hapa. Asante kwa umoja huu, Tunahisi msaada huu, na maamuzi yako mazito yalisaidia kulinda uhuru na demokrasia nchini Ukraine na kuwasaidia sana watu wa Ukraine’’ , amesema na kuongeza kuwa “Pia nataka kujadili na wewe leo maamuzi mazito ambayo yanaweza kutusaidia katika vita hivi,” Zelensky aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *