Alcaraz atwaa tena Ubingwa wa Wembledon dhidi ya Djokovic

Nyota wa mchezo wa Tenisi na aliyekuwa bingwa mtetezi wa taji la tennis la Wembledon Carlos Alcaraz raia wa Hispania ametwaa tena Ubingwa wa Michuano ya Wimbledon 2024 ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwake akimsafisha kwa seti zote 3-0 kwa ushindi wa seti 6-2, 6-2 na 7-6 dhidi ya mpinzani wake wa finali zilizopita Novak Djokovic.

Djokovic amesema, ana uhakika kijana huyo wa Kihispania ataendelea kunyakua Mataji makubwa ya mchezo huo kwasababu ana kila sifa za kuwa Bingwa wa mchezo huo.

Kwa upande wake Alcaraz anaamini ameshamaliza kazi kwa upande wa Tennis na sasa anakwenda kutazama ndugu zake wa Hispania watakaocheza fainali ya mpira wa miguu kombe la mataifa Ulaya (EURO 2024) dhidi ya Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *