Manchester United kumuajiri Andreas Georgson kama kocha wa ‘set-piece’

Kocha Msweden, Andreas Georgson ambaye aliwahi kufanya kazi na klabu ya Arsenal anatarajiwa kujiunga na Manchester United hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Norway ambako kocha huyo anafanya kazi na klabu ya Lillestrom, Manchester United imeanza mikakati ya kumnunua ili aje kuwa kocha wa ‘Set-piece’ klabuni hapo.

Taarifa zinasema kocha huyo anaweza kuigharimu Manchester United kiasi cha Pauni 280,000 (zaidi ya shilingi milioni 900 za kitanzania).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *