Yanga yaibamiza Kaizer Chiefs 4-0 kwao.

Klabu ya Yanga imeshinda goli 4-0 dhidi ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrka kusini kwenye mchezo wa fainali ya Toyota Cup ambao pia ni wa maandalizi ya msimu mpya uliochezwa kwenye dimba la Toyota Stadium mjini Bloemfontein Afrika kusini.

 

Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Mshambuliaji mpya Prince Dube, Stephanie Aziz Ki aliyefunga mawili na mshambuliaji kinda Clement Mzize.

 

Yanga baada ya mchezo huo watarejea jijini Dar es Salaam kwaajili ya maandalizi ya wiki ya Wananchi itakayofanyika Agosti 8 kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *