ALI KAMWE AJIUZULU NA KUAGA YANGA, AONDOKA RASMI

alikamwe

Aliyekuwa Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga Ali Kamwe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ametangaza kujiuzulu na kuaga mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kutumikia nafasi hiyo.

Hii inajiri baada ya Haji Manara kumaliza kifungo chake cha miaka miwili kujihusisha na masuala ya Michezo, Huku hata wakati Yanga imesafiri kuelekea Afrika Kusini, Ali Kamwe hakua sehemu ya waliosafiri na timu.

Huu hapa ujumbe wa Ali Kamwe kwa Mashabiki wa Yanga;
_______

A Good dancer must know when to Leave a Stage.

𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a 𝐽𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖..

Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;

Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani.

Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu.

Muda wangu umemalizika na Asanteni sana.

Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa.

DaimaMbeleNyumaMwiko.

Mwenyekiti wa Wasemaji
Ally Kamwe.

Yapi maoni yako?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *