Diamond aifikia rekodi ya Zuchu.

Video ya ngoma ya Jeje ya msanii Diamond Platnumz imefikisha watazamaji milioni 100 kwenye mtandao wa YouTube na kuwa video ya kwanza ya msanii huyo aliyoimba pekee yake kufikisha watazamaji milioni 100 Youtube akiwa msanii wa pili Tanzania na Afrika Mashariki.

Hivi karibuni video ya wimbo wa Sukari (2021) ya msanii Zuchu uliweka rekodi ya kufikisha watazamaji milioni 100 YouTube na kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki akiwa pia ni msanii aliye chini ya lebo ya WCB Wasafi.

Ikumbukwe kuwa ngoma ya Jeje mwaka 2020 iliongoza kutazamwa zaidi YouTube kwenye bara la Afrika ikimaliza mwaka na watazamaji zaidi ya milioni 40 huku msanii wa Nigeria Simi akishika nafasi ya pili kupitia video ya ngoma yake ya ‘Duduke’ iliyopata watazamaji zaidi ya milioni 29.

Ngoma za Bongo Fleva zenye watazamaji zaidi ya milioni 100 YouTube ni Kwangwaru (2018) wa Harmonize na Diamond, Yope Remix (2019) wa Diamond na Innoss’B, Inama (2019) wa Diamond na Fally Ipupa, Waah! (2020), Achii (2023) kolabo ya Diamond akiwa na Koffi Olomide.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *