Kagere alamba mkataba wa mwaka mmoja Namungo

Klabu ya Namungo imetangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba, Meddie Kagere kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake mkoani Lindi.

Kagere amesajiliwa mwaka mmoja baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Singida Black Stars kumalizika.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wamempa mwaka mmoja baada ya kuridhishwa na kile alichokifanya msimu uliopita.

“Tumemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja, awali alikuwa kwetu kwa mkopo akitokea Singida Fountain Gate ambayo sasa ni Singida Black Stars, amemaliza mkataba huko, tumejadiliana tumeona anatufaa hivyo tumemsajili, kwa maana hiyo Kagere bado ataendelea kucheza soka Tanzania,” kilisema chanzo kutoka Namungo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *