Ajali ya gari yaua mtalii hifadhi ya Serengeti

Mtalii mmoja amefariki na wengine 6 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea
jana Julai 28, 2024 saa 10 jioni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) leo Julai 29, 2024 gari hiyo ilikuwa na watalii 7 wenye asili ya China na dereva raia wa Tanzania.

Taarifa hiyo ilisomeka hivi;

“Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linapenda kuutaarifu umma kuwa jana majira ya saa 10 jioni gari la watalii lenye namba za usajili T603 DCL mali ya Kampuni ya
Yonda Africa lilipata ajali likiwa njiani kurudi hotelini kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Gari hiyo ilikuwa na watalii saba (7) wenye asili ya China na dereva raia wa Tanzania. Mgeni mmoja alifariki dunia, na wengine 6 walipata majeraha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mugumu na majeruhi sita wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo. Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka zingine ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *