Kupoteza kazi kwa Waziri kwaibua shangwe, vijana wakata keki kusherehekea
Kupoteza kazi kwa aliyekuwa Waziri wa Barabara wa nchini Kenya, Kipchumba Murkomen, kumekuwa sherehe kwa baadhi ya vijana almaarufu kwa jina la Gen Z wa huko North Rift nchini Kenya (iliko ngome ya waziri huyo). Ilikuwa furaha kwa baadhi ya vijana hao walioamua kufanya sherehe ya kukata keki kumshukuru Rais William Ruto kwa kumwachisha kazi…