Klabu ya Azam imepoteza 4-1 mchezo wao wa kirafiki dhidi ya klabu ya Wydad AC ya Morocco mchezo uliomalizika hivi punde.
Mchezo huo wa mwisho wa Azam kuhitimisha kambi yao ya Benslimane Morocco ulianza saa 2 usiku na kushuhudia sare ya 1-1 hadi mapumziko huku Azam wakibamizwa magoli matatu kipindi cha pili na vijana wa Rulani mokwena kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns.