Clara kama Ronaldo Al Nassr, afunga mawili wakishinda Ligi ya Mabingwa

clara

Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayekipiga katika klabu ya Al Nassr ya wanawake, Clara Luvanga jana amisaidia timu yake kushinda mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya klabu Bingwa Barani Asia kwa upande wa wanawake baada ya kufunga mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na timu yake katika mchezo wao dhidi ya klabu ya Myawady ya nchini Mynamar.

Kwenye mchezo huo wa kwanza kwa Al Nassr na Clara uliopigwa jana Agosti 25, 2024 wakiwa nyumbani, Al Nassr wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 na kujikita kileleni kwenye msimamo wa kundi A lenye jumla ya timu 4 kutoka mataifa manne tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *