Baba mzazi wa staa wa afrobeat kutoka Nigeria David Adeleke maarufu Davido bilionea Adedeji Adeleke siku ya jana ametoa sadaka ya fedha ya Kinigeria Bilioni 1 zaidi ya Bilioni 1 za Kitanzania kwenye kanisa la C&S aliloshiriki ibada ya kumuombea marehemu mama yake.
Bilionea huyo ametoa sadaka hiyo na kuikabidhi kwa uongozi wa kanisa baada ya kumalizika kwa ibada hiyo ya maombi ya kumuombea mama yake mzazi ambaye ni bibi wa Davido aliyefariki miaka kadhaa iliyopita.
Davido ameonyesha kufurahishwa na jambo hilo alilolifanya baba yake akieleza furaha yake kupitia Insta Story yake kwa kuchapisha kipande cha video hiyo na kuandika
“Baba yangu Mpendwa ananitia moyo kila siku, Nampenda huyu mtu hapa hapa”.